Ijumaa, 1 Novemba 2019

UKWELI KUHUSU MSHAHARA



1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku utakapoacha kuufanya mshahara wako mali ya ukoo ndipo siku mshahara huo utakuwa mkubwa! Hapo ndipo mshahara utatosha.
2. Siku utakapokuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya mshahara wako ndipo mshahara wako utakapotosha mahitaji yako ya kila mwezi.
3. Usiombe mwajiri wako akulipe overtime allowance, mwombe akupe muda wa kufanya kazi zako za ziada(perform your own overtime duties)
4. Epuka kuwasambazia pesa za mshahara wako watu wa ukoo wako ili uwaokoe na hali ngumu ya ukosefu wa fedha waliyonayo. Badala yake Wasaidie kuona fursa za kuwapatia Pesa!
5. Usiombe mwajiri wako akuongezee mshahara bali omba Mungu akuwezeshe Kupata kipato endelevu nje ya mshahara wako.
6. Mtu anayeishi kwa kutegemea mshahara wake tu ni sawa na mtu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga na mafuriko yalipokuja anguko la nyumba hiyo lilikuwa na mshindo mkubwa sana.
7. Mto Kagera au Maragalasi haijawahi kukauka maji yake. Kwa nini? Ni kwa sababu inapokea maji yake kutoka kwenye vyanzo vingi vya maji au vijito vingi! Mtu mwenye vyanzo vingi vya mapato zaidi ya mshahara atafanishwa na mto Kagera au Maragalasi isiyokauka maji yake.
8. Usisubiri kustaafu kazi ndipo ulipwe mamilioni ya pesa za kiinua mgongo bali tafuta kumiliki vyanzo sahihi vya pesa, na ndipo malipo ya kiinua mgongo utalipwa kila wiki mamilioni ya pesa.
9. Watu wenye busara hutafuta vyanzo vya pesa vinavyoweza kuwalipa mshahara au pensheni ya Tshs 150 milioni kwa mwezi badala ya kusubiri kulipwa kiinua mgongo cha Shs 150milioni baada ya kufanya kazi kwa miaka 30 au zaidi.
10. Waajiriwa wenye hekima na busara hutumia mishahara yao kutengeneza au kutandaza mabomba ya fedha au mtandao wa fedha endelevu ili hata kama hawatakuwepo tena duniani watoto wao na watoto wa watoto wao waendelee kupata mshahara kila mwezi!

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

\
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!
Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.
We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na SIKU NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi



Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka.
👇👇👇👇👇
Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Kazi Mara nyingi napenda kuifananisha na Ndoa, watu wengi walio nje ya kazi wanataka sana kazi na wakidhani ndiyo itakuwa mwanzo wa mafanikio yao.
Vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa ajira wanatamani waingie huko, lakini kutokana na ukweli kwamba kuna vitu hawavijui katika kazi ya kuajiriwa na ndio maana wanajihisi Wanyonge kwa kuto kuajiriwa.
*_USHAURI_*
kwanza tambua kukosa ajira siyo mkosi, wala siyo kwamba huna bahati. Yawezekana kwakukosa kwako ajira ni mlango wa kuwa muajiri. Unachotakiwa usilalamike tafuta fursa hapo ulipo, ndipo pana utajiri.
1. *_Kama hujaariwa acha kutamani maisha ya watu walio ajiriwa, ikiwezekana sitisha hata kupiga misele kwenye ofisi, zao kugongea maji ya dispenser_*
Badala yake anza kutafiti kwakina ni kwa namna gani watu ambao hawajaariwa wanaishi mtaani. Kuwa na marafiki wengi zaidi wanao pambana mtaani ili ujue wao wamewezaje.
*Tafuta ndege unao fanana nao*
2. *_Usidanganye kwamba ajira ndiyo itajibu matatizo yako yote unajidanganya_*
Badala yake kama utafanikiwa kupata iyo ajira, hakikisha unaifanya mbegu. Anza kwakuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji maana mshahara hauto kutosha kuishi maisha uliyo nayo kwenye akili yako.
Mwisho kabisa *_Nguvu na imani uliyoweka kwenye ajira iweke hivyo hivyo kwenye shughuli zako binafsi_*

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara


HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
💥Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.
💥Lakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.
💥Siku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa “Mlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.”.
💥Alivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.
💥Je huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?
💥Je unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!🙊
💥Kama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke.
Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang'anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUBORESHA MRADI WAKO


1»Tafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya
kuanza mradi wako
2»Usikate tamaa kwa changamoto/
misukosuko unayoweza kukutana nayo
njiani.
3»Ufanye mradi wako na mambo yote kwa
bidii kubwa
4»Jiwekee malengo ya wiki,mwezi na
mwaka
5»Uwe mbunifu na unayekubali kujifunza
mambo mapya na kukubali kubadilika
KUMBUKA-Soko ni kitu cha muhimu katika
mradi wako kwa sababu mwishoni
ukishapata mavuno yako kwa shughuli za
itahitaji uziuze hivyo kuwa makini na mradi
unaochagua kwa sasa miradi ambayo soko
lake ni rahisi kulipata ni Kuku wa kienyeji,
kuku wa mayai/nyama
matunda,mbaazi,ufuta n,k

SABABU ZA KUWA MJASIRIAMALI NA KUANZISHA MRADI/MIRADI


1-Mradi wako utapunguza gharama za
maisha
2
-Mradi wako utakufanya uwe kiongozi
[watu watakuiga na kufanikiwa].
3-Mradi wako utakufanya upate heshima
katika jamii.Mfano utaweza kujitosheleza
katika mahitaji yako yote -nyumba yako
,usafiri,n.k.
4
-Mradi wako utakuletea afya na uhakika
wa maisha .Mfano:ukipatwa na tatizo
utaweza kujitegemeya kwa sehemu kubwa
badala ya kuitegemea jamii.
5—-Mradi wako utaimarisha upendo kati
yako na wazazi wako kwani hutakuwa
tegemezi na pia utakuwezesha kuwasaidia.

NAMNA YA KUANZISHA MRADI

i»Ukishapata mtaji tulia na omba ushauri
kwa wazoefu juu ya mradi wako-uwe makini
na watu utakaowaomba ushauri.
ii»Fanya utafiti wa kutosha kuhusu mradi
wako,mfano utafiti wa masoko,usifanye
mradi kwa kuiga (kufuata mkumbo)
iii»Fanya mradi ambao unaupenda
iv»Fanya mradi ambao una ujuzi nao kama
hauna ujuzi nao unaweza kuanza kwa kiasi
kidogo
v»Hudhuria semina za kimaendeleo au
soma vitabu vya kukufanya uelewe namna ya
kuendeleza mradi huo.
vi»Fanya biashara halali na kama kubwa
kidogo inahitaji leseni basi itafute leseni
husika.