Ijumaa, 7 Agosti 2020

Mafunzo ya Biashara ya Forex.

 



Tumekuletea app mpya ynye masomo ya bishara ya forex, systems za kutrade forex pamoja na hints za kila siku.

Gusa kwenye link hapa chini kupakua app

Jumamosi, 25 Julai 2020

FURSA 6 ZA BIASHARA MTANDAONI BILA MTAJI













Hivi sasa teknolojia imekua ndio kila kitu hakuna mahali unapitia pasipo kutumia teknolojia, hiyo inadhirisha kuwa uwezekano wa kufanya biashara mtandaoni ni mkubwa sana cha msingi ni kujua ni vitu gani vya kufanya ili kuweza kuongeza kipato chako.

Kwa kuanza basi ni vyema nikwambie kabisa kuwa kama unataka kufanya biashara hizi mtandaoni, kama zilivyo biashara nyingine zinaitajika uwe mvumilivu na uwe unapenda kitu unachofanya tena ni vyema kutokufikiria pesa kwanza fanya kwanza unachokifanya kisha pesa itakuja baadae, kwa njia hiyo utaweza kufanya kitu hicho kwa uhakikia na bila kusimama au kuacha.
     
     1.Fungua Blog au Tovuti
Katika swala zima la kufungua blog au tovuti hapa ni mahali muhimu sana pakuzingatia kwani watu wengi huanzisha blog na baadae kuacha sababu tu mambo yamekua magumu au muda umekua mchache wakati mwingine unakuta mtu alifungua blog ya kitu asichokipenda au sababu aliona mtu mwingine alifungua blog ya aina flani na akafanikiwa.

Cha msingi hapa ni kutafuta kitu ambacho unakipenda kwa asilimia 100 na ukifanye bila kutegemea chochote kile kwani matokeo hua badae kabisa na inategemea na kitu unachokifanya na jinsi unavyo kifanya.

     2.Fungua Youtube Channel
Youtube ni mtandao ambao kujiunga ni bure kabisa, lakini pia ni sehemu ya kutengenezea pesa kama utakua unafanya kitu chenye mvuto kwa jamii pamoja na watu unaotaka kuwagusa kutokana na aina ya channel ambayo umefikiria kutengeneza.

Kwa hapa Tanzania kifupi ni kwamba watumiaji wa mtandao huo hawako wengi sana hivyo ni vizuri kufanya kitu ambacho ni bora kwa watu na kitavutia jamii kwa asilimia 100, hii pia inategemea na aina ya kitu unachofanya pamoja na ubora wa kitu unachofanya kumbuka pesa huja baadae hivyo fanya hivi kwa subira.

     3.Fanya Biashara ya Kutafuta Masoko (Online Marketing)
Kuna watu wengi sana wanafanya au wanafikiria kufanya matangazo kupitia Instagram, Facebook, Twitter, Google pamoja na Youtube watu hao wengi wao hawajui cha kufanya hivyo ukianzisha biashara ya mtandaoni ambayo itakuwa inahusika na kufanya matangazo kwenye sehemu hizo basi hakika utafanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Kufanya biashara hii unatakiwa kujitengenezea jina zuri pamoja na kuonyesha kwanini watu wakuchague wewe, hivyo ni vizuri kutumia muda wako kujijengea jina kwanza kabla ya kuanza kufanya biashara hii kwa hiyo pia biashara hii inaitaji subira.

     4.Fanya Kazi ya Kutafutia Kampuni Wateja (Affiliate)
Affiliate ni njia inayofahamika sana ya kufanya biashara mtandaoni kuna kampuni nyingi mtandaoni ziko tayari kutoa asilimia flani kutokana na wewe kumleta mteja mmoja, kuna mpaka kampuni zingine zinatoa asilimia 40 ya kipato kinacho patikana kwa mteja ulio mleta. Kufanya biashara hii unaitajika kuwa mtaalamu kidogo wa masoko na uwe na mtandao mkubwa wa watu ambao utaweza kuwa shawishi kununua bidhaa hizo ili kusababisha wewe kupata kamisheni.

      5.Tengeneza Akaunti za Mitandao ya Kijamii
Una njia imeingia sasa hasa kwenye mtandao wa Instagram njia ni yakutuma matangazo mbalimbali ya biashara kwenye akaunti mbalimbali, njia hii ni nzuri kama utakuwa umetengeneza akaunti ya kitu ambacho unakipenda na uhakikishe una weka makala mpya kila siku ili kuvutia follower wengi kwenye akaunti zako.

Hakikisha ununui follower kwa namna yoyote ile acha watu wakufuate wenyewe kwani akaunti nyingi zilizo nunua follower unakuta mtu ana post picha wana like watu 1000 wakati akaunti hiyo ina follower zaidi ya watu laki mbili, hapo unakuta hao 1000 ndio wenye kufuata page yako kutokana na kitu unachokifanya. Hivyo ni muhimu kufanya kitu unachokipenda na acha watu wakufollow wenyewe hapo utapata wateja wengi.
   

    6.Nunua na Uza Vitu Mtandaoni (Buy and Sell)
Kuna mitandao mingi hivi sasa ya kukupa uwezo wa kuuza vitu, unaweza kununua kitu kipya kisha ukakiuza kwenye mtandao au kama una kompyuta, simu au kitu chochote ambacho unaona huna matumizi nacho unaweza ukaanza kwa kukiuza kisha ukanunua tena na kuuza kwa faida.

Njia hii ni njia rahisi na inahitaji kuwa makini pale unapo nunua usije kununua kitu kibovu kwani biashara yako ndio inayotegemea, kuwa mvumilivu na hakikisha unafanya kwa umakini na ustarabu mkubwa sana ili kuongeza wateja kwenye biashara yako, pia hakikisha utafuti faida kubwa kwani hiyo itawafanya watu kuona ni bora waende dukani kuliko kununua kitu hicho kwako.

Hizo ni baadhi ya njia ambazo ukweli zinaweza kukusaidia kupata kipato na ukifuata kwa umakini utafanikiwa kwa asilimia 100, ukweli ni kwamba ukifanya unachokipenda lazima pesa na mafanikio yatakuja kwani utakifanya kwa ustarabu na umakini wa hali ya juu kwa sababu unakipenda hutaki kuona kitu hicho kiphicho oovyo. Hakikisha unafuata ndoto zako na anza kufanya sasa. 


Biashara ya Chips










JINSI YA KUANZISHA BIASHARA YA CHIPSI KWA TSH LAKI NNE NA THELASINI NA TANO 435,000. TU.
Biashara ya chipsi imezidi kushamiri na kuwa moja Kati ya chakula pendwa Sana hivyo kupelekea kuwa ajira na sehemu ya kipato kwa watu.
Leo nataka kukuonyesha namna unaweza kuanza biashara yako kwa mtaji mdogo tu wa laki nne na ukaiona faida.
GHARAMA ZA KUDUMU.
Jiko la chips......................... 30,000.
Jiko la mishkaki...............25,000-45,000.
Kabati la vioo....................200,000.
Sahani kumi (10).......15,000.
meza ndogo ......50,000.
Vikorokoro vya kusaidia kazi ...30,000.
Ndoo unaweza kutumia za kwako si lazima ununue.
GHARAMA ZA KUENDESHA BIASHARA.
Kodi........5000 kila siku pengine 3000.
Mkaa.......7000.
Ndoo ya viazi............15,000.
Kuku wawili..........10,000.
mafuta 3 litre....@14000.
mayai Trey moja. 8000.
JUMLA KUU .......435,000.
KUMBUKA: BEI HIZI ZINABADILIKA KULINGANA NA SOKO.




Ijumaa, 1 Novemba 2019

Siri ya mafanikio katika maisha: Usiangalie watu



Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea"
▪Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha, tambua kwamba unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu
▪ _watakaokuvunja moyo_ ,
▪ _watakaokusema vibaya_ ,
▪ _watakaokukatisha tamaa._
▪ _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.
▪Mara nyingi sana unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya , kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).
▪Wakati mwingine utashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
▪mtu mmoja alisema "siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu".
▪Tambua kwambwa huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani "hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi", yaani ilimradi tu wakupinge.
▪Itazame hatima yako.


Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.
2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako.
Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.
Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako- Basi ww usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa
3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia.
Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.
4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.
Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.
Maarifa ndio mtaji wa kwanza.
Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, "Omba ndoano, usiombe samaki"
5. Usitunze mbegu badala ya kuipanda.
Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza.
Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa.Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa”
6. Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.
Unapomkopesha mtu huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake-halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope”
7. Usikubali kumdamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini.
Kumbuka- dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa
8. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo.
Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni.
Ili kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako.
Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama”
9. Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.
Maeneo kama kwenye soksi, sidiria, chini ya mto wa kulalia, chini ya begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama.
~Ni rahisi kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa zako.
Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.
10. Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako.
Jiulize kwanza kabla hujanunua,
"Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah?”
Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.
12. Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako.
Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.
Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.
Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.
13. Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.
Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo.
Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa.
Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto.
Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa.
Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.
*Mwendo*

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.

Kufanikiwa kwenye maisha ni matokeo ya kujua
mambo sahihi ya kuyafanya.Ni kama ilivyo wakati
unapotaka kufungua mlango
uliofungwa,unachohitaji ni ufunguo sahihi wa
kutumia na sio vinginevyo.
Ili ufanikiwe lazima uwe mtu mwenye bidii na
ambaye unawathamini watu bila kujali hali zao za
sasa.Ili kutoka hapo ulipo na kwenda kule
unakotaka unahitaji watu wa kukuunganisha na
fursa mpya,kukuonyesha njia nzuri ya kufanya
mambo,wa kukurekebisha na watu ambao
unaweza kujifunza kwao.

Mwaka 2012 mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa
vya michezo ya Modell nchini marekani,bwana
Mitchell Modell alifanya tukio la ajabu sana lililotoa
funzo kubwa la mafanikio katika maisha yetu ya
kila siku.Aliamua kujibadilisha mwonekano wake
kwa kunyoa nywele zake zote na kuweka ndevu
nyingi sana za bandia na pia kuvaa hereni sikio
moja.Kisha baada ya hapo alienda kuomba kazi
kwenye kampuni yake na akaanza kufanya kazi ya
daraja la chini kabisa.
Akiwa ameajiriwa bila watu kujua kuwa ndiye
mmiliki alikutana na wafanyakazi wengi sana wa
aina mbalimbali.Kati ya wafanyakazi katika tawi lile
alikuwepo dada mmoja anayeitwa Angel ambaye
alikuwa ana watoto 3 ila hakuwa anakaa na mume
wake na kwa muda wa miaka 2.Lakini pia,Angel na
watoto wake wamekuwa wanaishi kwenye vibanda
kwani hakuweza kulipia pango kwenye nyumba
nzuri ya kuishi.Gharama zote za
chakula,ada,matibabu na mavazi ya watoto yote
ilikuwa juu yake.
Pamoja na hali yake hiyo,Angel alikuwa ni
mfanyakazi anayewahi kazini kila siku na alikuwa
anafanya kazi kwa bidii sana.Hata wakati wengine
walikuwa wanalamika juu ya mshahara,yeye kazi
yake ilikuwa ni kuwatia moyo na kuwahamasisha
wafanye kazi kwa bidii sana akiamini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri.Kila wakati Bwana
Mitchell alipokuwa anamkuta Angel,alikuta
anafanya kazi zake kwa umakini na hata akikuta
anaongea na wenzake basi itakuwa ni kuwatia
moyo na kuwapa hamasa na kuwataka waaache
kulalamika.
Wakati Bwana Mitchell akiwa kama mfanyakazi
mpya alihitaji sana msaada wa kufundishwa jinsi
mfumo unavyofanya kazi na mambo mengine.Kila
mmoja alikuwa hayuko tayari kumfundisha,ila
Angel alikuwa tayari kumfundisha na kumsaidia
hata na kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya
kutokana na ugeni wake.Na kwa sababu ya ukaribu
wake ndipo alipoweza kumfahamu Angel na
kuyajua maisha yake kwa undani.
Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila mtu
yoyote kujua kuwa ndiye mmiliki,ndipo alipoamua
kufanya kitu kikubwa kwa Angel.Kwanza
alimpandisha cheo na kumfanya kuwa meneja
msaidizi na kisha alimpa zawadi ya dola laki mbili
na hamsini(Takribani shilingi milioni 500 za
kitanzania) ili aweze kupata nyumba nzuri ya
kuishi.
Baada ya tukio hili kutokea wafanyakazi wengi
sana walijilaumu na walitamani sana kupata fursa
upya kama wangejua kuwa yule alikuwa ni mmiliki.
Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo safari ya
mafanikio ilivyo.mara zote huwezi kujua ni wakati
gani fursa kubwa inayohusu maisha yako
itakutokea.Kilichomfanya Angel kufanikiwa ni ile
hali ya kuwa ni mtu ambaye hakuruhusu jambo
lolote limzuie kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi
kila wakati hata kipindi ambacho maisha yake
yalikuwa magumu.
Mara nyingi unaweza kujikuta katika hali ambazo
zinakatisha tamaa na zinakupa uhalali wa kila
namna wa wewe kuwa mtu wa kulalamika na
kukata tamaa.Hebu fikiria mama wa watoto
watatu,analipwa mshahara mdogo lakini bado
anawahi ofisini na huwa halalamiki.Kuna fursa
nyingi kwenye maisha unazikosa kwa sababu ya
malalamiko juu ya hali inayokuzunguka.Kitu cha
msingi unachotakiwa kujua ni kuwa kulalamikia
kitu au mtu hakuwezi kubadilisha hali yako ya sasa
lakini kufanya kwa bidii kunaweza kufungua fursa
nyingi kubwa katika maisha yako.
Inawezekana kazi unayoifanya ni ndogo
ukilinganisha na ndoto kubwa
uliyonayo,inawezekana mshahara unaolipwa sio
mkubwa kama unavyotaka,inawezekana biashara
yako bado haifanyi vizuri kama mipango yako
ilivyo ama hauna mtaji kiwango
unachotaka.Katikati ya hali hii unachotakiwa
kufanya sio kuanza kulalamika na kukata
tamaa,unatakiwa kuwa kama Angel,weka kiwango
kikubwa cha bidii kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajifungulia milango mikubwa zaidi
katika maisha yako.
Kuanzia leo fanya maazimio katika maisha yako
kuwa utakuwa mtu wa kufanya kwa bidii kile
ambacho unakifanya hata kama itakuwa kwenye
mazingira magumu,kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitengenezea fursa kubwa sana mbele
yako.Ukiamua kuishi kwa mtazamo huu,muda
mfupi sana ujao utafanikiwa.
Kitu kingine cha msingi cha kukizingatia hapa ni
kuwa usidharau watu katika maisha yako.Kati ya
mafumbo makubwa ambayo Mungu ameyafumba
ni kuhusu hatima za watu ambao tunakutana nao
kila siku katika maisha yetu.Hakuna kitu kibaya
kama kumdharau mtu eti kwa sababu anaonekana
kwa wakati huo hawezi kukusaidia
chochote.Jifunze kumuheshimu na kumthamini
kila mtu.
Ilil ufanikiwe katika maisha yako jifunze kuishi
kama Angel,jifunze kuwa na bidii ya kazi hata
katika mazingira magumu lakini pia jifunze
kuthamini kila mtu ambaye unakutana naye-
Kuanzia mdada wa kazi
nyumbani,mlinzi,mfagizi,kondakta wa daladala
hadi dereva wako.Kila mtu ni muhimu na ana
mchango katika maisha yako.Kanuni ya maisha
inasema-“Husiana na watu kama wewe unavyotaka
watu wengine wahusiane na wewe pia”. Kuanzia leo
ishi na kila mtu kama “Mitshell wako” wa
kukuunganisha na fursa kubwa uliyokuwa
unaisubiria.
Sina shaka kuwa fursa yako kubwa iko njiani
inakuja,usikate tamaa.
Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,

Kauli 10 za mtu ambaye unatakiwa umuepuke maishani

Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu
1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu
5)Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6) Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7)Kupata ni majaliwa
8)Usilazimishe mambo
9)Kuna watu special siyo mimi.
10)Sina bahati
KAA MBALI NA HUYO MTU. NI HATARI KWA NDOTO ZAKO!!!!