Ijumaa, 1 Novemba 2019

Siri ya mafanikio katika maisha: Usiangalie watu



Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea"
▪Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha, tambua kwamba unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu
▪ _watakaokuvunja moyo_ ,
▪ _watakaokusema vibaya_ ,
▪ _watakaokukatisha tamaa._
▪ _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.
▪Mara nyingi sana unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya , kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).
▪Wakati mwingine utashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
▪mtu mmoja alisema "siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu".
▪Tambua kwambwa huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani "hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi", yaani ilimradi tu wakupinge.
▪Itazame hatima yako.


Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.
2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako.
Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.
Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako- Basi ww usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa
3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia.
Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.
4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.
Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.
Maarifa ndio mtaji wa kwanza.
Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, "Omba ndoano, usiombe samaki"
5. Usitunze mbegu badala ya kuipanda.
Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza.
Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa.Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa”
6. Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.
Unapomkopesha mtu huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake-halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope”
7. Usikubali kumdamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini.
Kumbuka- dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa
8. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo.
Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni.
Ili kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako.
Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama”
9. Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.
Maeneo kama kwenye soksi, sidiria, chini ya mto wa kulalia, chini ya begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama.
~Ni rahisi kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa zako.
Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.
10. Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako.
Jiulize kwanza kabla hujanunua,
"Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah?”
Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.
12. Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako.
Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.
Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.
Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.
13. Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.
Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo.
Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa.
Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto.
Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa.
Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.
*Mwendo*

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.

Kufanikiwa kwenye maisha ni matokeo ya kujua
mambo sahihi ya kuyafanya.Ni kama ilivyo wakati
unapotaka kufungua mlango
uliofungwa,unachohitaji ni ufunguo sahihi wa
kutumia na sio vinginevyo.
Ili ufanikiwe lazima uwe mtu mwenye bidii na
ambaye unawathamini watu bila kujali hali zao za
sasa.Ili kutoka hapo ulipo na kwenda kule
unakotaka unahitaji watu wa kukuunganisha na
fursa mpya,kukuonyesha njia nzuri ya kufanya
mambo,wa kukurekebisha na watu ambao
unaweza kujifunza kwao.

Mwaka 2012 mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa
vya michezo ya Modell nchini marekani,bwana
Mitchell Modell alifanya tukio la ajabu sana lililotoa
funzo kubwa la mafanikio katika maisha yetu ya
kila siku.Aliamua kujibadilisha mwonekano wake
kwa kunyoa nywele zake zote na kuweka ndevu
nyingi sana za bandia na pia kuvaa hereni sikio
moja.Kisha baada ya hapo alienda kuomba kazi
kwenye kampuni yake na akaanza kufanya kazi ya
daraja la chini kabisa.
Akiwa ameajiriwa bila watu kujua kuwa ndiye
mmiliki alikutana na wafanyakazi wengi sana wa
aina mbalimbali.Kati ya wafanyakazi katika tawi lile
alikuwepo dada mmoja anayeitwa Angel ambaye
alikuwa ana watoto 3 ila hakuwa anakaa na mume
wake na kwa muda wa miaka 2.Lakini pia,Angel na
watoto wake wamekuwa wanaishi kwenye vibanda
kwani hakuweza kulipia pango kwenye nyumba
nzuri ya kuishi.Gharama zote za
chakula,ada,matibabu na mavazi ya watoto yote
ilikuwa juu yake.
Pamoja na hali yake hiyo,Angel alikuwa ni
mfanyakazi anayewahi kazini kila siku na alikuwa
anafanya kazi kwa bidii sana.Hata wakati wengine
walikuwa wanalamika juu ya mshahara,yeye kazi
yake ilikuwa ni kuwatia moyo na kuwahamasisha
wafanye kazi kwa bidii sana akiamini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri.Kila wakati Bwana
Mitchell alipokuwa anamkuta Angel,alikuta
anafanya kazi zake kwa umakini na hata akikuta
anaongea na wenzake basi itakuwa ni kuwatia
moyo na kuwapa hamasa na kuwataka waaache
kulalamika.
Wakati Bwana Mitchell akiwa kama mfanyakazi
mpya alihitaji sana msaada wa kufundishwa jinsi
mfumo unavyofanya kazi na mambo mengine.Kila
mmoja alikuwa hayuko tayari kumfundisha,ila
Angel alikuwa tayari kumfundisha na kumsaidia
hata na kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya
kutokana na ugeni wake.Na kwa sababu ya ukaribu
wake ndipo alipoweza kumfahamu Angel na
kuyajua maisha yake kwa undani.
Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila mtu
yoyote kujua kuwa ndiye mmiliki,ndipo alipoamua
kufanya kitu kikubwa kwa Angel.Kwanza
alimpandisha cheo na kumfanya kuwa meneja
msaidizi na kisha alimpa zawadi ya dola laki mbili
na hamsini(Takribani shilingi milioni 500 za
kitanzania) ili aweze kupata nyumba nzuri ya
kuishi.
Baada ya tukio hili kutokea wafanyakazi wengi
sana walijilaumu na walitamani sana kupata fursa
upya kama wangejua kuwa yule alikuwa ni mmiliki.
Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo safari ya
mafanikio ilivyo.mara zote huwezi kujua ni wakati
gani fursa kubwa inayohusu maisha yako
itakutokea.Kilichomfanya Angel kufanikiwa ni ile
hali ya kuwa ni mtu ambaye hakuruhusu jambo
lolote limzuie kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi
kila wakati hata kipindi ambacho maisha yake
yalikuwa magumu.
Mara nyingi unaweza kujikuta katika hali ambazo
zinakatisha tamaa na zinakupa uhalali wa kila
namna wa wewe kuwa mtu wa kulalamika na
kukata tamaa.Hebu fikiria mama wa watoto
watatu,analipwa mshahara mdogo lakini bado
anawahi ofisini na huwa halalamiki.Kuna fursa
nyingi kwenye maisha unazikosa kwa sababu ya
malalamiko juu ya hali inayokuzunguka.Kitu cha
msingi unachotakiwa kujua ni kuwa kulalamikia
kitu au mtu hakuwezi kubadilisha hali yako ya sasa
lakini kufanya kwa bidii kunaweza kufungua fursa
nyingi kubwa katika maisha yako.
Inawezekana kazi unayoifanya ni ndogo
ukilinganisha na ndoto kubwa
uliyonayo,inawezekana mshahara unaolipwa sio
mkubwa kama unavyotaka,inawezekana biashara
yako bado haifanyi vizuri kama mipango yako
ilivyo ama hauna mtaji kiwango
unachotaka.Katikati ya hali hii unachotakiwa
kufanya sio kuanza kulalamika na kukata
tamaa,unatakiwa kuwa kama Angel,weka kiwango
kikubwa cha bidii kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajifungulia milango mikubwa zaidi
katika maisha yako.
Kuanzia leo fanya maazimio katika maisha yako
kuwa utakuwa mtu wa kufanya kwa bidii kile
ambacho unakifanya hata kama itakuwa kwenye
mazingira magumu,kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitengenezea fursa kubwa sana mbele
yako.Ukiamua kuishi kwa mtazamo huu,muda
mfupi sana ujao utafanikiwa.
Kitu kingine cha msingi cha kukizingatia hapa ni
kuwa usidharau watu katika maisha yako.Kati ya
mafumbo makubwa ambayo Mungu ameyafumba
ni kuhusu hatima za watu ambao tunakutana nao
kila siku katika maisha yetu.Hakuna kitu kibaya
kama kumdharau mtu eti kwa sababu anaonekana
kwa wakati huo hawezi kukusaidia
chochote.Jifunze kumuheshimu na kumthamini
kila mtu.
Ilil ufanikiwe katika maisha yako jifunze kuishi
kama Angel,jifunze kuwa na bidii ya kazi hata
katika mazingira magumu lakini pia jifunze
kuthamini kila mtu ambaye unakutana naye-
Kuanzia mdada wa kazi
nyumbani,mlinzi,mfagizi,kondakta wa daladala
hadi dereva wako.Kila mtu ni muhimu na ana
mchango katika maisha yako.Kanuni ya maisha
inasema-“Husiana na watu kama wewe unavyotaka
watu wengine wahusiane na wewe pia”. Kuanzia leo
ishi na kila mtu kama “Mitshell wako” wa
kukuunganisha na fursa kubwa uliyokuwa
unaisubiria.
Sina shaka kuwa fursa yako kubwa iko njiani
inakuja,usikate tamaa.
Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,

Kauli 10 za mtu ambaye unatakiwa umuepuke maishani

Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu
1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu
5)Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6) Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7)Kupata ni majaliwa
8)Usilazimishe mambo
9)Kuna watu special siyo mimi.
10)Sina bahati
KAA MBALI NA HUYO MTU. NI HATARI KWA NDOTO ZAKO!!!!

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Na ndio maana kwenye maisha, mafanikio ya leo ni matokeo ya tulichojifunza kutoka kwa waliopita, baada ya wao kukosea mahali nasi tukaboresha, na kwa hakika vizazi vijavyo navyo vitaendelea kurekebisha pale tunapokosea sisi na hii yote ndiyo huleta ladha ya maisha. Ukipitia Changamoto mwenyewe na ukapambana kujikwamua mwenyewe, utapata somo litakalokufunza zaidi kuliko kusimuliwa changamoto walizopiti wengine.
Maisha ni Maamuzi, aliyekula Sahani mbili za wali mchana ili usiku asile tena, anaweza kuwa sawa na aliyeamua kutokula Mchana ili usiku ale sahani mbili za wali, japo hawa hawawezi kuwa sawa sawia na aliyeamua kula sahani moja ya wali mchana na moja ya wali usiku, Ijapokua mwisho wa siku wote wamekula sahani Mbili za wali kwa siku. Jumapili Njema kwenu nyote.
JIKUNG'UTE….JIPANGE…..ANZA……

Mafanikio ya maisha sio Elimu tuu



MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.
👉🏾Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa
🙇🏽📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 🚙magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)
👉🏾Wapo 🙇🏽📚wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana
👉🏾Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga
Hii inachangiwa na mambo mawili:-
👇🏽
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli
👉🏾Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio
👉🏾Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!
🙇🏽📚Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
👇🏾
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!
👉🏾Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.
✋🏾Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
🤔Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani
🛣Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti
😎Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze
😀🙏🏽 Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze

LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI



Karibuni;
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na
kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na
kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika
Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya
na Makampuni mbalimbali.
5. ** Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya
electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na
vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. ** Kuuza software; mfano Antivirus, Operating
Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks,
batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo,
Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na
vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. ** Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza
popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta
na zinazotumia mafuta
16. ** Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na
hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. ** Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. ** Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za
mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa
vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na
miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building
contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua
(solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya
solar n.k
34. ** Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. ** Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters,
HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa
vingine.
40. ** Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. ** Kufungua kampuni ya kutoa huduma za
internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. ** Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au
mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. ** · Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi,
Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku,
Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. ** · Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na
kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. ** Kuchimba/Kuuza Madini
56. ** Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na
fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. ** Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika
sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. ** Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na
magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. ** Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding
machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. ** Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha
wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya
redio na televisheni
79. ** Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV
Games)
80. ** Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na
winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. ** Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali
zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom,
TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. ** Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe,
mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa
barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha,
kutoboa na kuchana mbao
92. ** Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme
wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. ** Kukodisha matenki ya maji**
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA,
TIGOPESA, EZY PESA
100. ** Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi
(Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,
vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. ** Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya
anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. ** Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa
kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. ** Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. ** Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. ** Kununua nyumba katika Maghorofa
(Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. ** Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. ** Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo
KAMA YOTE HAYA UMESHINDWA KUPATA LA
KUFANYA, WEWE UTAKUWA USHAPOTEA,
ENDELEA NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU
SERIKALI. MABADILIKO YANAANZIA KWAKO

Tabia za kuepuka ili uweze kuwa tajiri


UKIWA NA HIZI TABIA 9, JIANDAE KUFA MASKINI…………
By Kashindi Edson
"Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu" (Nelson Mandela, R.I.P)
"Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio"(Mwl Nyerere, R.I.P).
"Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako"(Mahatma Gandhi, R.I.P)
"Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa"(Bill Gate, The richest man in the world).
Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, "mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini". Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.
Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;

1. KUTOKUJARIBU.

Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. "Chagua kufa, au kupambana". "Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

2. KUTOKUJIFUNZA.

Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. "JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

3. WOGA & WASIWASI.

"Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana"(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

4. KUJILINGANISHA.

Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.**

"Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine". Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

6. UONGO

"Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele"(WEUSI), "Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini"(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. "Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote"(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

7. UVIVU & UZEMBE

"Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero"(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno "kazi" katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. "Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae".

8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA

Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. "Sisi ni kile tunacho kula". Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako". Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. "Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana"(Nikki Mbishi,).

9. LAWAMA & UMBEA

"Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu" We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la "wachawi". Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.
—-= Unaweza kuwa umekataliwa katika ajira moja kumbe kuna ajira nyingine tena yenye maslahi zaidi inakusubiri.
—-= Umekataliwa na mteja mmoja na kumbe kuna wateja wengi wanakusubiri.
—-= Umekataliwa katika chuo kimoja mwaka huu kumbe mwakani kuna nafasi yako inakusubiri.
——= Umekataliwa na mpenzi ulioamini kabisa atakua wako wa maisha kumbe aliye wako haswaa anakusubiri ufike.
Watu wengi kinachowarudisha nyuma, "ni kuacha kuboresha fikra zao ili kuwa watatuzi wa matatizo_(problem solvers)_ ila wameamua kuwa walalamikaji tu kila siku, ili tuendelee ni lazima tujikite katika kutafuta majibu ya matatizo yanayotuzunguka." Yaani, mara zote jiulize " *sasa nifanye nini? Na sio kwa nini mimi?"*
Mtaalamu mmoja aliwahi kusema " _Life is 10% of what happens to you and 90% of how you respond to it_". Yaani _yale yanayokutokea maishani yanachangia asilimia kumi tu kuboresha au kuharibu maisha yako na asilimia 90 ya maisha yako ni jinsi wewe unavyoyachukulia maisha hayo_. Kwa nini ukate tamaa baada ya kukataliwa. Yape maisha yako maana sana thamani ya juu kabisa ili kukataliwa kwako iwe ni kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Tambua utakacho na unachoweza kukifanya. Jifunze vizuri na ubobee ili kuuhakikishia ulimwengu kwamba wewe sio mzigo ila ni sehemu ya wenye majibu ya matatizo yanayotuzunguka.
Kukataliwa, ni mtaji. Kila jambo lina wakati wake

UKWELI KUHUSU MSHAHARA



1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku utakapoacha kuufanya mshahara wako mali ya ukoo ndipo siku mshahara huo utakuwa mkubwa! Hapo ndipo mshahara utatosha.
2. Siku utakapokuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya mshahara wako ndipo mshahara wako utakapotosha mahitaji yako ya kila mwezi.
3. Usiombe mwajiri wako akulipe overtime allowance, mwombe akupe muda wa kufanya kazi zako za ziada(perform your own overtime duties)
4. Epuka kuwasambazia pesa za mshahara wako watu wa ukoo wako ili uwaokoe na hali ngumu ya ukosefu wa fedha waliyonayo. Badala yake Wasaidie kuona fursa za kuwapatia Pesa!
5. Usiombe mwajiri wako akuongezee mshahara bali omba Mungu akuwezeshe Kupata kipato endelevu nje ya mshahara wako.
6. Mtu anayeishi kwa kutegemea mshahara wake tu ni sawa na mtu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga na mafuriko yalipokuja anguko la nyumba hiyo lilikuwa na mshindo mkubwa sana.
7. Mto Kagera au Maragalasi haijawahi kukauka maji yake. Kwa nini? Ni kwa sababu inapokea maji yake kutoka kwenye vyanzo vingi vya maji au vijito vingi! Mtu mwenye vyanzo vingi vya mapato zaidi ya mshahara atafanishwa na mto Kagera au Maragalasi isiyokauka maji yake.
8. Usisubiri kustaafu kazi ndipo ulipwe mamilioni ya pesa za kiinua mgongo bali tafuta kumiliki vyanzo sahihi vya pesa, na ndipo malipo ya kiinua mgongo utalipwa kila wiki mamilioni ya pesa.
9. Watu wenye busara hutafuta vyanzo vya pesa vinavyoweza kuwalipa mshahara au pensheni ya Tshs 150 milioni kwa mwezi badala ya kusubiri kulipwa kiinua mgongo cha Shs 150milioni baada ya kufanya kazi kwa miaka 30 au zaidi.
10. Waajiriwa wenye hekima na busara hutumia mishahara yao kutengeneza au kutandaza mabomba ya fedha au mtandao wa fedha endelevu ili hata kama hawatakuwepo tena duniani watoto wao na watoto wa watoto wao waendelee kupata mshahara kila mwezi!

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

\
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!
Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.
We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na SIKU NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi



Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka.
👇👇👇👇👇
Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Kazi Mara nyingi napenda kuifananisha na Ndoa, watu wengi walio nje ya kazi wanataka sana kazi na wakidhani ndiyo itakuwa mwanzo wa mafanikio yao.
Vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa ajira wanatamani waingie huko, lakini kutokana na ukweli kwamba kuna vitu hawavijui katika kazi ya kuajiriwa na ndio maana wanajihisi Wanyonge kwa kuto kuajiriwa.
*_USHAURI_*
kwanza tambua kukosa ajira siyo mkosi, wala siyo kwamba huna bahati. Yawezekana kwakukosa kwako ajira ni mlango wa kuwa muajiri. Unachotakiwa usilalamike tafuta fursa hapo ulipo, ndipo pana utajiri.
1. *_Kama hujaariwa acha kutamani maisha ya watu walio ajiriwa, ikiwezekana sitisha hata kupiga misele kwenye ofisi, zao kugongea maji ya dispenser_*
Badala yake anza kutafiti kwakina ni kwa namna gani watu ambao hawajaariwa wanaishi mtaani. Kuwa na marafiki wengi zaidi wanao pambana mtaani ili ujue wao wamewezaje.
*Tafuta ndege unao fanana nao*
2. *_Usidanganye kwamba ajira ndiyo itajibu matatizo yako yote unajidanganya_*
Badala yake kama utafanikiwa kupata iyo ajira, hakikisha unaifanya mbegu. Anza kwakuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji maana mshahara hauto kutosha kuishi maisha uliyo nayo kwenye akili yako.
Mwisho kabisa *_Nguvu na imani uliyoweka kwenye ajira iweke hivyo hivyo kwenye shughuli zako binafsi_*

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara


HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
💥Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.
💥Lakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.
💥Siku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa “Mlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.”.
💥Alivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.
💥Je huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?
💥Je unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!🙊
💥Kama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke.
Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang'anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUBORESHA MRADI WAKO


1»Tafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya
kuanza mradi wako
2»Usikate tamaa kwa changamoto/
misukosuko unayoweza kukutana nayo
njiani.
3»Ufanye mradi wako na mambo yote kwa
bidii kubwa
4»Jiwekee malengo ya wiki,mwezi na
mwaka
5»Uwe mbunifu na unayekubali kujifunza
mambo mapya na kukubali kubadilika
KUMBUKA-Soko ni kitu cha muhimu katika
mradi wako kwa sababu mwishoni
ukishapata mavuno yako kwa shughuli za
itahitaji uziuze hivyo kuwa makini na mradi
unaochagua kwa sasa miradi ambayo soko
lake ni rahisi kulipata ni Kuku wa kienyeji,
kuku wa mayai/nyama
matunda,mbaazi,ufuta n,k

SABABU ZA KUWA MJASIRIAMALI NA KUANZISHA MRADI/MIRADI


1-Mradi wako utapunguza gharama za
maisha
2
-Mradi wako utakufanya uwe kiongozi
[watu watakuiga na kufanikiwa].
3-Mradi wako utakufanya upate heshima
katika jamii.Mfano utaweza kujitosheleza
katika mahitaji yako yote -nyumba yako
,usafiri,n.k.
4
-Mradi wako utakuletea afya na uhakika
wa maisha .Mfano:ukipatwa na tatizo
utaweza kujitegemeya kwa sehemu kubwa
badala ya kuitegemea jamii.
5—-Mradi wako utaimarisha upendo kati
yako na wazazi wako kwani hutakuwa
tegemezi na pia utakuwezesha kuwasaidia.

NAMNA YA KUANZISHA MRADI

i»Ukishapata mtaji tulia na omba ushauri
kwa wazoefu juu ya mradi wako-uwe makini
na watu utakaowaomba ushauri.
ii»Fanya utafiti wa kutosha kuhusu mradi
wako,mfano utafiti wa masoko,usifanye
mradi kwa kuiga (kufuata mkumbo)
iii»Fanya mradi ambao unaupenda
iv»Fanya mradi ambao una ujuzi nao kama
hauna ujuzi nao unaweza kuanza kwa kiasi
kidogo
v»Hudhuria semina za kimaendeleo au
soma vitabu vya kukufanya uelewe namna ya
kuendeleza mradi huo.
vi»Fanya biashara halali na kama kubwa
kidogo inahitaji leseni basi itafute leseni
husika.