Ijumaa, 31 Mei 2019

Njia 7 za kujipatia mtaji wa biashara

Njia za kupata Mtaji wa biashara: Baada ya kuamua kuingia kwenye biashara/ ujasiriamali, sasa unahitaji mtaji wakufanyia na kukuzia biashara yako.
Mambo muhimu kuyajua:
Sio kila biashara inahitaji mtaji au mtaji mkubwa!
Kuna biashara zingine unahitaji tu kufahamiana na watoa bidhaa au huduma basi. Mfano biashara ya bodaboda, unahitaji tu kufahamiana na mwenye boda boda wewe unafanya kazi kwanza halafu unapeleka sehemu ya makubaliano yako na tajiri baadaye
Hata kama biashara yako itahitaji mtaji mkubwa unaweza siku zote funja funja hayo malengo ya biashara katika ngazi ambayo unaweza anza na mtaji unaoweza kumudu kuupata.
Mfano unaweza kuwa unataka kuwa na hoteli kubwa ya biashara. Hapa unaweza anza na mgahawa na baadaye ikakua
Mfano wa pili
Labda unataka kuwa na supermarket, unaweza anza na mtaji wa 10,000 kuunza vitunguu, chumvi kwa nyumba za jirani mpaka ufukishe mwaka utakuwa na mtaji mkubwa ajabu.
Kama biashara yako itahitaji mtaji kwanza fikiria mambo manne (4) yafuatayo
  1. Aina ya biashara (Kuzalisha, kuchuuza, huduma)
  2. Aina ya soko (kipato kidogo, wanawake tu, wanaume tu, watoto tu, vijana tu, kijiji au mtaa tu nk)
  3. Ukubwa wa mtaji (Mdogo, wa kati au mkubwa?)
  4. Ufahamu wako kwenye biashara yako – Elimu/Ujuzi nk
Majibu ya maswali hapo juu ndio itakayoamua wewe upate mtaji wapi
Sasa swali, wapi utapata huo mtaji nk.
Mlolongo huu hapa chini utakusaidia kujua ni wapi utapata huo mtaji wa biashara.
1. Mali Binafsi
Kama una shamba, fedha, nyumba, gari, mifugo, mazao nk unaweza kutumia mali hizi kama mtaji wa biashara
Kumb. Ukishakubali kuwa mfanyabiashara wewe utakuwa daima ni mtu wa kununua na kuuza. Kwa hiyo hata kitanda chako unachokipenda sana kwa wakati fulani unaweza lazimika ukiuze ili upate mtaji wa biashara. Muhimu usiingie kichwa kichwa kwenye biashara na kujiletea hasara.
Faida: Haina riba, hata ikitokea bahati biashara ikafilisika haiwezi filisi na mali zingine kwani hakuna dhamana ya mali yako.
Hasara: Hakuna msukumo wa biashara kwani mhusika hajali hata akipata hasara, Hivyo ni vigumu kupata faida na biashara kukua.
2. Wabia wa Biashara
Saa nyingine unatakiwa kuwatumia watu wengine ili kupata yafuatayo
  1. Mtaji wa mali
  2. Mtaji wa mawazo na fikra tofauti
Wabia wa baishara yako inaweza ongeza kasi ya kukua kwa biashara kwani fikra tofauti inaweza kuwa chachu ya maendeleo ya biashara husika ukiachilia mbali mtaji ambao wabia wako watakuja nao.
Inabidi lakini uwachague kwa uangalifu mkubwa wabia wako kwani wengine wanaweza kuwa ni wavurugaji na sio wa kuaminiwa.
Faida: Kuongezeka kwa kasi ya kukua kwa biashara kwa sababu ya fikra tofauti
Hasara: Mifarakano yenye kuweza kuua biashara ni dhahiri
3. Wawekezaji wa Biashara
Wawekezaji ni watu ambao wanaweza toa mali na pesa zao kukuwezesha wewe kufanya biashara yako lakini wao watahitaji baada ya muda wa uwekezaji warudishiwe pesa au mali zao na riba mliokubaliana kwenye mktaba wa uwekezaji.
Faida: Uhakika wa mtaji na hivyo uhakika wa kufanya biashara
Hasara: Biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa
4. Mkopo Kutoka kwa Watu wa Karibu
Ndugu/jamaa/marafiki na majirani wanaweza kuwa ni chanzo kizuri ya mtaji usio nariba.
Wanaweza kukupa fedha taslimu, wanyama, vitu kama mashine, mitambo, nyumba, ardhi, gari, kompyuta, na vifaa mbalimbali
Faida: Ni rahisi kupata mkopo bila mlolongo wa masharti, uwezekano wa kufilisiwa ni mdogo au hakuna kabisa
Hasara: Kwa vile ni mkopo wa ndugu/jamaa, jirani na marafiki, hakuna msukumo wa kufanya biashara kwa sababu hakuna kufilisiwa hivyo ni ngumu kupata faida na pia kukua kwa biashara yako
5. Mkopo Kutoka Kwenye Vyama, Vikundi nk
Vyama vya kijamii, kitaaluma, vikundi vya kuweka na kukopa, Vikoba vinaweza kuwa chanzo cha karibu kupata mkopo wa biashara wenye riba na masharti nafuu. Unachotakiwa tu ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.
Faida: Uhakika wa mtaji japo unaaza na mdogo, uanweza kuepuka kufilisiwa mali zako. Kunakuweo na msukumo kwa kiwango fulani ya kufanya biashara na hivyo uwezekano wa kupata faida na biashara yako kukua
Hasara: Mtaji ni mdogo pale unapooanza
6. Mkopo Kutoka Kwenye Mashirika ya fedha (Micro-Credit Enterprises)
Mashirika kama Pride Tanzania, Vision Tanzania (zamani ikiitwa SEDA), Finca, Faida nk ni hatua nzuri kwa biashara ndogo kwani nao kama ilivyo vikoba wanatoa mikopo midogo kwa masharti nafuu.
Faida: Mlolongo mdogo, dhamana ni rahisi, wanaelimisha
Hasara: Riba ni kubwa, biashara ikifeli utafilisiwa mali ulizoweka dhamana
7. Mkopo kutoka Benki na Tasisi kubwa za Fedha
Mkopo unaohusisha benki ni sharti iwe ni biashara kubwa na mhusika awe na uhakika na soko pamoja na mtaji kurudi.
Mabenki mengine wanatoa mikopo mikubwa na midogo kwa pamoja.
Faida: Uhakika wa kupata mkopo mkubwa, pia msukumo wa kufanya biashara ni mkubwa na hivyo uwezekano mkiubwa wa kutengeneza faida
Hasara: Mlolongo wa kuupata ni mrefu, Kwa bahati mbaya biashara ikifeli, unafilisiwa haraka mali uliyoweka dhamana
Masharti ya mkopo
–          Dhamana kama vile nyumba, arthi, mazao, kikundi n.k.
–          Mchanganuo wa biashara
–          Biashara inayo endelea(<miaka 3)
–          Kuwepo kwa ofisi kama ni mkopo mkubwa zaidi ya milioni 3
–          Biashara iliyosajiliwa kam ni biashara kubwa
–          Riba ya mkopo
–          Kiasi cha mkopo na uwezo wa mkopo
–          Muda wa kurudisha mkopo na riba

Jumanne, 28 Mei 2019

Mwanzo wa kufa biashara yako



Je ni biashara ngapi zinazoanzishwa na kufa kila mwaka?

Kwa wastani mfano zikianzishwa biashara 100 kwa mwaka basi biashara zitakazovuka mwaka ni chini ya 20.Hivyo kila mwaka 80% ya  biashara mpya zinakufa kabla ya kufikisha mwaka.

Je ni mambo gani yanayosababisha kufa kwa biashara kabla ya mwaka wa kwanza?

1.Elimu ndogo ya biashara.

"Mali bila daftari huisha bila habari", kukosekana kwa tarakimu na kumbukumbuku katika biashara ni jambo linalosababisha biashara kufa.Lazima ujue umeingiza shilingi ngapi na umetumia shilingi ngapi.Kukosekana kwa mapato na matumizi ndio mwazo wa kula mtaji bila kujua,wewe utaona biashara inaenda ila ukikaa kupiga hesabu utaona kuna kiashiria cha kupungua mtaji.

2.Kukosekana kwa moyo wa kijasiriamali.

Hili nalo ni tatizo kubwa,baadhi ya watu wanadhani wakianzisha biashara basi faida itapatikana kirahisi.Endapo kukawa na faida ndogo ukilinganisha na matarajio hapo ndipo mtu hukata tamaa,na ndio mwazo wa kufa kwa biashara. Jambo muhimu ni kwamba katika biashara yoyote lengo ni kupata faida,hata iwe ndogo kiasi gani ili mradi gharama za uendeshaji zinapatikana.

3.Kutomudu ushindani.

Ukishindwa kumudu ushindani uliopo ni tatizo kubwa.Endapo mwenzako anatengeneza bidhaa moja na wewe hakikisha bei yako iwe ndogo na uzidi ubora wake.Ukiwaza faida tu katika biashara yako hautoweza kumudu ushindani hivyo biashara yako ipo hatiani kufa.

4.Huduma mbovu kwa wateja.

Mapato makubwa utayapata ni jinsi gani unamhudumia mteja wako.Biashara yako inaweza kuwa nzuri ila tatizo likawa kwa wahudumu wako.Kinachotokea hapa ni kwamba mteja wako lazima ahame na kutafuta sehemu yenye huduma kwa wateja nzuri.Hapa tunazungumzia biashara ambazo 100% zinahitaji kutolewa na mhudumu na sio biashara za mtandao ambazo mara nyingi zinatumia automations.

5.Huduma mbovu bei kubwa.

Biashara kutoka China zinafanya vizuri kutokana na bei ndogo, japokuwa baadhi ya bidhaa zake sio bora.Wewe unachotakiwa kufanya ni kutoa huduma bora kwa bei ya chini,hapa kutakuwezesha kupata wateja wote wa kipato cha chini mpaka juu.Suala sio kuangalia faida kinachotakiwa kwanza ni kuua ushindani kisha kukuza jina.

6.Anza kuendesha biashara kitigitali.

Njia za kusaka wateja zinazidi kuwa tofauti tofauti.Ukitegemea mteja akufuate mpaka dukani mwenyewe mambo yanabadilika.Lazima uanze kujitangaza kwa njia za kidigitali kuweza kuvuta wateja wapya.Usipofanya hivyo wateja wapya utawapata kwa nadra na hata ulionao watapungua.Hapa ndipo mwanzo wa biashara yako kulegalega na hatimae kufa.Hakuna ujanja mwingine kwenye biashara zaidi ya kujipanga wewe mwenyewe na kujua unawavutiaje wateja.



Jumatatu, 27 Mei 2019

Biashara ya Matunda

BIASHARA YA MATUNDA(FRUIT SALAD)

Mahitaji
Vifaa
Epron@sh3000-5000
Kilemba au kofia maalum@sh1000-3000
Kisu @sh1000-3000
Beseni @sh1500-3000
Slicer(mashine ya kukatia matunda)@sh15,000-350000
Container(vifungashio)@sh100-150
Vijiko na uma vya plastic @sh50-100
Maji na sabuni @1000

Malighafi
Machungwa@sh100-150
Matango@sh200-500
Maembe@sh300-500
Ndizi@sh60-150
Nanasi@sh500-1500
Strawberry@sh5000kg
Zabibu@sh1000-2500
Parachichi@sh200-500
Papai@sh1000-2500
Tikiti maji@sh3000-10000
N.k

JINSI YA KUANDAA MATUNDA
Matayarisho
1. Osha na ondoa maganda kwenye embe, nanasi,ndizi,tango, papai na tikiti,parachichi,papai, maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba
2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake, katakata strawberry katika vipande vidogo
3.Osha vifungashio kwa maji ya moto viache vikauke majimaji yote waweza vifuta kwa vitambaa safi
3.kisha weka kwa mgawanyo sawa wa vipande katika vifungashio vyako
3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo, kama huna friji nunua barafu livunje vunje weka saladi yako kwa saa 1
4. Saladi yako tayari kwa kuliwa
Waweza kuuza katika maduka,ofisi,vyuo,stendi na sehemu zenye makutano ya watu wengi pia inaweza kuliwa kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku
5.bei ya container moja ya fruit salad ni sh 700-1500 kulingana na mazingira uliyopo
6.mtaji ni kuanzia Tsh 100,000
7.ili kuboresha biashara na kuitofautisha unaweza tengeneza kajarida kadogo kitakacho elezea faida za kila tunda kwa mwili na tiba yake kwa magonjwa

Angalizo bei ya vitu inatofautiana kulingana na mahali ulipo.

Chukua hatua mjenzi wa maisha yako ni wewe mwenyewe

Ijumaa, 24 Mei 2019

Biashara ya Mgahawa (Cafeteria)




Kefteria ni mradi au biashara inayohusiana na uuzaji wa vyakula na vinywaji katika eneo maalumu  kwa  lengo  la  kujipatia  kipato  na  kutoa  huduma  katika  jamii  husika  na inayokuzunguka. Mradi huu huusisha wafanyakazi na sio mtu mmoja peke yako kwa maana unaingiliana na vitengo mbalimbali kama upishi, uandaaji wa vyinywaji, mhudumu wa kusikiliza wateja na mnunuzi wa bidhaa pindi zitakapoisha, hivyo zingatia idadi ya watu utakaowashirikisha kabla ya kuanza mradi, kumbuka mradi huu sio lazima uumiliki wewe katika vitengo vyote bali unaweza kutoa fursa kwa mtu kushikilia kitengo cha kuuza juisi au vyakula vya kubeba kama chipsi ili kuboresha eneo la biashara kua na mandhari ya mvuto.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kufanikisha kufunga eneo lako la biashara hii:-

1.  Kuandika mpango wa biashara. Fanya hivi bila kujali  aina  ya biashara  unakusudia  kufungua ni ndogo, mpango wa biashara ni muhimu kama hatua ya kwanza katika  mchakato wakibiashara. mpango mzuri wa biashara husaidia uchambuzi wa biashara yako,  soko lake, na mpango wake kwenda mbele kwa miaka kadhaa.
Jinsi ya kuandika Mpango wa Biashara kwa taarifa za kina juu ya mchakato. Kwa mfano, vipengele kawaida ya mpango wa biashara ni pamoja na:

  Kichwa cha habari na Orodha ya Yaliyomo.
  Maelezo ya ufupisho, ambayo ni muhtasari wa maono yako kwa ajili ya biashara.
  Maelezo ya ujumla. Ni maelezo ambayo wewe hutoa maelezo ya jumla ya biashara  yako na aina ya huduma utakazotoa kwa soko lake.
  Bidhaa na Huduma, ambayo wewe kuelezea, kwa kina, bidhaa yako ya kipekee au  huduma.
  Mpango wa Masoko, ambayo wewe kueleza jinsi ya kuleta bidhaa yako kwa wateja  wake.
  Mpango wa utendaji, ambayo wewe kueleza jinsi biashara itakuwa ikiendeshwa kwa  msingi wa siku hadi siku.
  Usimamizi na ushirika, ambapo unaweza kufafanua muundo wa watu katika biashara  yako na falsafa ambayo inasimamia yake.
  Mpango wa kifedha, ambapo wewe utaonyesha mfano wako wa kufanya kazi kwa  ajili ya fedha na mahitaji yako kutoka kwa mtaji ulionao.

2.  Mahitaji ya kisheria, na usalama wa biashara. Kuanzisha cafe pia inahusisha mambo ya
kisheria kama usajili wa biashara na tozo za kodi. lakini pia afya na usalama ni mahitaji ya ziada ya sekta ya chakula.

3.  Kuweka biashara yako utambulisho. Hii inahusisha jina na nembo ya biashara yako
itakayotumika katika utoaji wa huduma ili uweze kujitangaza kirahisi kwa watu wengi. 4. Uchunguzi na ukusanyaji wa wateja. Hii inahusisha wateja wa cafe yako kulingana na  uchunguzi wako na utafiti wa jamii yako na jirani kulingana na malengo ya biashara  yako. Je, ni wafanyakazi wa ofisi? Chuo ? makutano au umati wa watu, au sehemu watu  hukaa na kuangalia mipira au kwa mazungumzo ya utulivu? Habari hii kusaidia kuongoza  biashara yako pia.

5.  Eneo la biashara. Kuchunguza maeneo kadhaa tofauti ambayo yanaendana na bidhaa
zako. Angalia katika maeneo mbalimbali ambayo pia malighafi zako zinapatikana kirahisi .Kuchagua mahali bora ambapo pia inaendana na bajeti yako na hutoa eneo bora kwa wateja. Kama imekuwa awali kutumika kama cafe, hii inaweza kufanya kazi kwa
manufaa yako kwa sababu huwezi haja ya kutumia muda na fedha kusafiri kwajili ya  kununua malighafi. Bila shaka, fikiria kwa nini kwamba cafe iwepo hapo. 6. Ratiba ya ufanyaji biashara. Hii huusisha kua unapangilia muda gani kufungua hadi  kufunga café yako ili kuwapa wateja urahisi wa kuwahi na kuja kwa wakati katika eneo  lako.

7.  Kupata vifaa zinahitajika kuendesha cafe yako. unaweza kuwa na uwezo wa kutumia
baadhi zilizozoeleka kama meza, viti, friji, majiko, kabati ya vyakula na vyombo. Hata hivyo, bila ya shaka hainahaja ya kununua vifaa vyote kama bajeti haitoshi, badala yake unaweza kukodisha angalau baadhi ya vifaa vinavyotahitaji.

8.  Akiba ya malipo, hii huusisha fedha za kulipia umeme na maji kwa siku za mwanzo kabla
faida haijakua nzuri kutokana na matuminzi ya umeme na maji kuwa mengi sana katika biashara za vyakula

9.  Vifaa boreshi na pendezeshi, hivi ni vitu ambavyo utaweza kuviweka ili kuvutia wateja
wako wa kila siku mfano, sabuni ya maji, maji yamoto, kapeti za meza, tishu, vipande vidogo vya matunda.

10. Kujenga orodha yako ya bidhaa, hii ni muongozo au menyu ya aina ya vyakula na  vinywaji ambavyo hutolewa kwenye café yako ili kumrahisishia mteja kuweza kuchagua  kiurahisi kitu au chakula anachotaka.

11. Ujuzi na utaalamu, hakikisha unakua na uelewa juu ya uandaaji wa bidhaa zako za  vyakula au vinywaji kiutaalamu ili kuzingatia ubora wa hali ya juu ,kama itakua huna
utaalamu huo itakulazimu kuajiri wapishi wenye uzoefu na utaalamu ili kukuandalia bidhaa zako kiutaalamu na ubora

12. Kuanzisha uhusiano na wauzaji na wasambazaji. Unahitaji kupata bidhaa bora na kwa  gharama nafuu zaidi kutoka kwa wasambazaji na vitu vingine unavyohitaji kuendesha  biashara yako ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, unahitaji kujenga mahusiano imara na  wauzaji wa kuaminika ambao mara kwa mara utapata ubora wa vyakula na menus mpya  (miongoni mwa mambo mengine mengi) na wewe utarahisisha muda na kwa bei nzuri.

13. Uzoefu wa biashara ya cafe ni ya muhimu na manufaa, ni vyema kulipa angalau kama  kipaumbele kwa Kufanya mahojiano ya kina, na kuuliza maswali kwa watu walioanza na  wenye uzoefu wa muda mrefu

14. Fungua biashara wakati umekamilisha na upo tayari. Mara kila kitu ikiwa kimekamilika  na biashara yako ni tayari kwa ajili ya kuanza, kufungua milango na anza biashara yako  kwa kualika watu.

         

Alhamisi, 23 Mei 2019

Mobile Saloon za Kiume

MOBILE BARBER SHOP
Nimetumia jina maarufu, lakini najua wengi mnafahamu kuwa namaanisha saluni ya kiume. Biashara ya saluni ya kiume ni kubwa na imepanuka. Ni biashara ya uhakika kwa sababu kati ya mambo muhimu mjini watu wanayozingatia ni usmart.
Kama wewe ni kinyozi hili ni dili zuri kwako. Siyo kila mtu ana muda. Wengine wana fedha lakini hawana muda. Kuna watu wanapenda kunyoa nywele, ndevu na huduma nyingine za saluni kama kufanya steaming, waves, black, facial, scub nk kila wiki lakini hawana muda wa kwenda saluni.
Changamkia hii dili. Kazi yako ni kununua mashine zako mbili na vifaa vingine vya kawaida, kisha unapachika jina mathalani JULIUS MOBILE BARBER SHOP. Utapiga pesa nzuri sana.
Kumbuka kwa sababu ni huduma ya kumfuata mtu kwake, bei haitakuwa ileile. Kwa wastani (kwa aina ya watu ninaowazungumzia hapa) bei ya kunyoa saluni ni wastani wa Tsh. 5000 (nywele na ndevu) kwa saluni nyingi za mijini.
Hapo bado scub, waves na huduma nyingine kama atapenda ambazo kwa watani mteja mmoja hugharamia si chini ya Tsh. 10,000. Ukimfuata kwake, itakuwa mara mbili au tatu na pengine ukalipwa zaidi kulingana na utakavyotoa huduma.
Kuna wagonjwa, wazee na watoto ambao ndugu zao hawataki usumbufu wa kuwapeleka saluni. Kuwa mjanja kwa kuchungulia hii fursa.

Ufugaji wa Nguruwe

ELIMU YA UJASILIAMALI JUU YA UFUGAJI WA NGURUWE

MCHANGANUO MDOGO WA MRADI WA NGURUWE
-Nguruwe watoto 20 @ 20,000 = 400,000
– Banda la mabanzi=1,000,000
– Chakula = 1,000,000
– Dawa= 200,000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000.
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike).
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500.
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda chuo cha sokoine (SUA) na vyuo vingine vya kilimo na mifugo ukaonane na wataalamu au tembelea maofisa ugani na wataalam mbalimbali wa mifugo au wafugaji wenye uzoefu.
ZIJUE KANUNI KUU NNE KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE.
Je unazifahamu aina za nguruwe na sifa zake,
Zifuatazo ni aina za nguruwe zinazo fungwa kwa wingi  nchini Tanzania ambazo pia mfugaji yeyote anaweza kufuga kwani upatikanaji wake ni rahisi kwa maeneo yaliyo mengi.
Large white.
Nguruwe hawa wana rangi nyeupe mwili mzima
Masikio yao yanakuwa yamesimama mda wote.
Nyuso zao zimeingia kwa ndani kidogo (muonekano wake upo kama dish)
Saddleback
Wakubwa tofauti na aina nyingine za nguruwe.
Masikio yamelala kiasi
Landrace
Wana ukubwa wa wastani
Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mbele.
Mara baada ya kuzijua aina za nguruwe na sifa zake, sasa zijue kanuni za msingi katkia ufugaji wa nguruwe.
Mambo ya msingi kwa ufugaji wa nguruwe.
– Chagua koo zinazo zalisha vyema.
Uchaguzi wa koo huchangia zaidi ya asilimia 80 katika mafanikio ya ufugaji wa nguruwe, chagua koo amabayo ina  zalisha watoto wengi na wenye afya.
Kwa mfugaji ambaye anataraji kununua nguruwe kutoka kwa mfugaji mwingine, Zingatia sana kumbukumbu zilizo wekwa na mfugaji yule na cha msingi ziwe sahihi hii itakupa picha ya kujua uzazi wa nguruwe huyo.
– Jenga banda bora.
Jenga banda ambalo linaendana na idadi na ukubwa wa nguruwe, banda ambalo halitapitisha mwanga mkali wa jua, upepo mkali,pia litakalo himimili mikimiki ya nguruwe wakorofi, hii itasaidia kupunguza usumbufu na bugudha kwa nguruwe na hatazalisha bila shida kwa nguruwe anayeishi katika nyumba yenye bugudha na usumbufu uzalishaji wake upungua sana uzalushaji.
– Zingatia afya bora kwa nguruwe.
Sote tunafahamu afya ni kitu cha msingi sana iwe kwa binadamu na hata mnyama hivyo, Afya bora ya nguruwe ni kitu cha msingi sana kuzingatiwa kwa kwa nguruwe asiye na afya bora udhoofika na uzalishaji wake hushuka kwa kiwango kikubwa sana..
Afya bora hutokana na kufanya, Chanjo dhidi ya magonjwa kama minyoo.
– Walishe wanyama chakula bora.
Chakula cha nguruwe ni muhimu kiandaliwe kulingana ma umri wa
nguruwe na mahitaji katika mwili wa nguruwe
Chakula cha nguruwe kiwe katika uwiano sahihi hii, chakula ambacho kita kidhi mahitaji ya mwili na uzakushaji kuwa mkubwa.
Nguruwe hapatiwe chakula chenye vyanzo vya madini, vitamin na protini.
Vyakula venye vyanzo vya protini husaidia sana katika kujenga mwili.
Vitamin na madini vyakula venye vyanzo hivi vinahitajika kwa wigni hasa calcium na phosphorus kwa nguruwe wa kunenepesha na walioachishwa kunnyonya.
Epuka kuwapa nguruwe kuwapa chakula chenye chumvi nyingi kwani hii itamfanya nguruwe kunywa maji mengi sana na matokeo yake nguruwe huarisha sana natimaye ukuaji wake huwa wa polepole. Hata hivyo kumbuka chumvi uongeza radha ya chakula na uwekaji wake katika mchanganyo wa chakula uwe ni asilimia 0.5 tu