Ijumaa, 31 Mei 2019

Njia 7 za kujipatia mtaji wa biashara

Njia za kupata Mtaji wa biashara: Baada ya kuamua kuingia kwenye biashara/ ujasiriamali, sasa unahitaji mtaji wakufanyia na kukuzia biashara yako.
Mambo muhimu kuyajua:
Sio kila biashara inahitaji mtaji au mtaji mkubwa!
Kuna biashara zingine unahitaji tu kufahamiana na watoa bidhaa au huduma basi. Mfano biashara ya bodaboda, unahitaji tu kufahamiana na mwenye boda boda wewe unafanya kazi kwanza halafu unapeleka sehemu ya makubaliano yako na tajiri baadaye
Hata kama biashara yako itahitaji mtaji mkubwa unaweza siku zote funja funja hayo malengo ya biashara katika ngazi ambayo unaweza anza na mtaji unaoweza kumudu kuupata.
Mfano unaweza kuwa unataka kuwa na hoteli kubwa ya biashara. Hapa unaweza anza na mgahawa na baadaye ikakua
Mfano wa pili
Labda unataka kuwa na supermarket, unaweza anza na mtaji wa 10,000 kuunza vitunguu, chumvi kwa nyumba za jirani mpaka ufukishe mwaka utakuwa na mtaji mkubwa ajabu.
Kama biashara yako itahitaji mtaji kwanza fikiria mambo manne (4) yafuatayo
  1. Aina ya biashara (Kuzalisha, kuchuuza, huduma)
  2. Aina ya soko (kipato kidogo, wanawake tu, wanaume tu, watoto tu, vijana tu, kijiji au mtaa tu nk)
  3. Ukubwa wa mtaji (Mdogo, wa kati au mkubwa?)
  4. Ufahamu wako kwenye biashara yako – Elimu/Ujuzi nk
Majibu ya maswali hapo juu ndio itakayoamua wewe upate mtaji wapi
Sasa swali, wapi utapata huo mtaji nk.
Mlolongo huu hapa chini utakusaidia kujua ni wapi utapata huo mtaji wa biashara.
1. Mali Binafsi
Kama una shamba, fedha, nyumba, gari, mifugo, mazao nk unaweza kutumia mali hizi kama mtaji wa biashara
Kumb. Ukishakubali kuwa mfanyabiashara wewe utakuwa daima ni mtu wa kununua na kuuza. Kwa hiyo hata kitanda chako unachokipenda sana kwa wakati fulani unaweza lazimika ukiuze ili upate mtaji wa biashara. Muhimu usiingie kichwa kichwa kwenye biashara na kujiletea hasara.
Faida: Haina riba, hata ikitokea bahati biashara ikafilisika haiwezi filisi na mali zingine kwani hakuna dhamana ya mali yako.
Hasara: Hakuna msukumo wa biashara kwani mhusika hajali hata akipata hasara, Hivyo ni vigumu kupata faida na biashara kukua.
2. Wabia wa Biashara
Saa nyingine unatakiwa kuwatumia watu wengine ili kupata yafuatayo
  1. Mtaji wa mali
  2. Mtaji wa mawazo na fikra tofauti
Wabia wa baishara yako inaweza ongeza kasi ya kukua kwa biashara kwani fikra tofauti inaweza kuwa chachu ya maendeleo ya biashara husika ukiachilia mbali mtaji ambao wabia wako watakuja nao.
Inabidi lakini uwachague kwa uangalifu mkubwa wabia wako kwani wengine wanaweza kuwa ni wavurugaji na sio wa kuaminiwa.
Faida: Kuongezeka kwa kasi ya kukua kwa biashara kwa sababu ya fikra tofauti
Hasara: Mifarakano yenye kuweza kuua biashara ni dhahiri
3. Wawekezaji wa Biashara
Wawekezaji ni watu ambao wanaweza toa mali na pesa zao kukuwezesha wewe kufanya biashara yako lakini wao watahitaji baada ya muda wa uwekezaji warudishiwe pesa au mali zao na riba mliokubaliana kwenye mktaba wa uwekezaji.
Faida: Uhakika wa mtaji na hivyo uhakika wa kufanya biashara
Hasara: Biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa
4. Mkopo Kutoka kwa Watu wa Karibu
Ndugu/jamaa/marafiki na majirani wanaweza kuwa ni chanzo kizuri ya mtaji usio nariba.
Wanaweza kukupa fedha taslimu, wanyama, vitu kama mashine, mitambo, nyumba, ardhi, gari, kompyuta, na vifaa mbalimbali
Faida: Ni rahisi kupata mkopo bila mlolongo wa masharti, uwezekano wa kufilisiwa ni mdogo au hakuna kabisa
Hasara: Kwa vile ni mkopo wa ndugu/jamaa, jirani na marafiki, hakuna msukumo wa kufanya biashara kwa sababu hakuna kufilisiwa hivyo ni ngumu kupata faida na pia kukua kwa biashara yako
5. Mkopo Kutoka Kwenye Vyama, Vikundi nk
Vyama vya kijamii, kitaaluma, vikundi vya kuweka na kukopa, Vikoba vinaweza kuwa chanzo cha karibu kupata mkopo wa biashara wenye riba na masharti nafuu. Unachotakiwa tu ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.
Faida: Uhakika wa mtaji japo unaaza na mdogo, uanweza kuepuka kufilisiwa mali zako. Kunakuweo na msukumo kwa kiwango fulani ya kufanya biashara na hivyo uwezekano wa kupata faida na biashara yako kukua
Hasara: Mtaji ni mdogo pale unapooanza
6. Mkopo Kutoka Kwenye Mashirika ya fedha (Micro-Credit Enterprises)
Mashirika kama Pride Tanzania, Vision Tanzania (zamani ikiitwa SEDA), Finca, Faida nk ni hatua nzuri kwa biashara ndogo kwani nao kama ilivyo vikoba wanatoa mikopo midogo kwa masharti nafuu.
Faida: Mlolongo mdogo, dhamana ni rahisi, wanaelimisha
Hasara: Riba ni kubwa, biashara ikifeli utafilisiwa mali ulizoweka dhamana
7. Mkopo kutoka Benki na Tasisi kubwa za Fedha
Mkopo unaohusisha benki ni sharti iwe ni biashara kubwa na mhusika awe na uhakika na soko pamoja na mtaji kurudi.
Mabenki mengine wanatoa mikopo mikubwa na midogo kwa pamoja.
Faida: Uhakika wa kupata mkopo mkubwa, pia msukumo wa kufanya biashara ni mkubwa na hivyo uwezekano mkiubwa wa kutengeneza faida
Hasara: Mlolongo wa kuupata ni mrefu, Kwa bahati mbaya biashara ikifeli, unafilisiwa haraka mali uliyoweka dhamana
Masharti ya mkopo
–          Dhamana kama vile nyumba, arthi, mazao, kikundi n.k.
–          Mchanganuo wa biashara
–          Biashara inayo endelea(<miaka 3)
–          Kuwepo kwa ofisi kama ni mkopo mkubwa zaidi ya milioni 3
–          Biashara iliyosajiliwa kam ni biashara kubwa
–          Riba ya mkopo
–          Kiasi cha mkopo na uwezo wa mkopo
–          Muda wa kurudisha mkopo na riba

Maoni 3 :

  1. asante kwa elimu nzuri
    mambo ya msingi sana yanaerimisha mno
    samahani nanaswali kama huto jari
    NINASHAUKU YA KUFUNGUA ACOUNT BANK LAKINI NASHINDWA KUTAMBUA NI BENKI IPI INAFAA KWA HUDUMA BORANA KUMJARI MTEJA

    JibuFuta
  2. Iko wazi kila mtu ana uwezo wa kuielewa inakatisha tamaa hasa mikopo mikubwa

    JibuFuta
  3. Kwa hakika umeandika vizur sana katika kupanuwa mawazo ya mtu

    JibuFuta