Ijumaa, 1 Novemba 2019

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

\
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!
Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.
We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na SIKU NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

Maoni 1 :

  1. tunashukuru kwa topic zenu nzuri sana:wapo watu wenye mitaji yao mfano wa wastani mil 5 lakini kulingana na mazingira unakuta biashara nyingi zinafanana ,lakini akitaka atafte biashara tofauti na zilizopo anakutana na changamoto ya ubunifu ,je mutu huyu mnamshaurije ikiwa anataka awe na biashara ambayo haipo katika eneo hilo

    JibuFuta