![](https://fbs.com/upload/promo/banner/6fc0da51b018149ada47cd109944b707.gif?ppu=13940898)
Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea"
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea"
▪Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha, tambua kwamba unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu
▪ _watakaokuvunja moyo_ ,
▪ _watakaokusema vibaya_ ,
▪ _watakaokukatisha tamaa._
▪ _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.
▪ _watakaokuvunja moyo_ ,
▪ _watakaokusema vibaya_ ,
▪ _watakaokukatisha tamaa._
▪ _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.
▪Mara nyingi sana unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya , kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).
▪Wakati mwingine utashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
▪mtu mmoja alisema "siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu".
▪mtu mmoja alisema "siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu".
▪Tambua kwambwa huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani "hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi", yaani ilimradi tu wakupinge.
▪Itazame hatima yako.
![](https://fbs.com/upload/promo/banner/241a1e5e9a9925d241107026b7e65de0.gif?ppu=13940898)
Kwakweli katika maisha mtu pekee anaeweza kukuunga mkono katika Hali zako zote ni wewe mwenyewe
JibuFutaNdio ilivyo hivyi
JibuFutaNi hakika ya mambo haya muhim nikulenga kule unataka kufika nna kumwamini MUNGU
JibuFuta